Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 23:45

Rais aliyepinduliwa Mali ajiuzulu


People stand as waves from the Bay of Bengal approach the shore in Visakhapatnam district in the southern Indian state of Andhra Pradesh on October 12, 2013.
People stand as waves from the Bay of Bengal approach the shore in Visakhapatnam district in the southern Indian state of Andhra Pradesh on October 12, 2013.

Wapatanishi wa ECOWAS wanasema walipokea barua ya kujiuzulu kutoka kiongozi huyo Jumapili.

Rais Amadou Toumani Toure, amewambia waandishi wa habari baada ya kujitokeza kwa mara ya kwanza Jumapili, kutoka mahali alipokua anajificha tangu mapinduzi ya mwezi uliyopita , kwamba amechukua hatua hiyo bila ya kulazimishwa, bali kwa sababu ya kuisaidia nchi yake.

Hatua yake hivi sasa inaruhusu mahakama kuu ya Mali kutangaza kwamba kiti cha rais ni kitupu na hivyo kuruhusu kumteua rais wa mpito, katika juhudi za kurudisha nchi hiyo katika utawala wa kisheria na mfumo wa demokrasia.

Viongozi wa kijeshi walochukua madaraka baada ya mapinduzi ya Marchi 21, walitia mkataba na Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS, siku ya Ijumaa kukubali kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.

Miongoni mwa makubaliano ni kumteua Spika wa bunge Dioncounda Traoré, kuwa rais wa mpito na kuongoza serikali itakayo tayarisha uchaguzi mkuu.

ECOWAS imeahidi kuisaidia Mali kupambana na waasi wa Tuareg walochukua udhibiti wa sehemu kubwa ya kaskazini ya nchi hiyo na kutangaza uhuru wa taifa lao wiki iliyopita.

Majirani wa Mali wamekosoa vikali mapinduzi ya kijeshi na kutangazwa kwa taifa jipya la Azwad na waasi wa kaskazini walopata msaada kutoka kundi la wanaharakati wa kislamu la Ansar.

XS
SM
MD
LG