Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 20:21

Raila, Ruto wahutubia mikutano ya mwisho ya kampeni kabla ya uchaguzi mkuu Jumanne


Willian Ruto and Raila Odinga
Willian Ruto and Raila Odinga

Wagombea urais nchini Kenya, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga na Naibu wa Rais William Ruto, Jumamosi walihutubia mikutano yao ya mwisho ya kampeni mjini Nairobi kwelekea kwa uchaguzi mkuu Jumanne wiki ijayo.

Odinga anayepeperusha bendera ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya na viongozi wa mrengo huo pamoja na wafuasi wao, walikusanyika katika uwanja wa michezo wa Kasarani huku Ruto, anayewania kwa tikiti ya chama cha UDA chini ya muungano wa Kenya Kwanza akijiunga na wenzake kwenye uwanja wa Nyayo.

Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi, Jumamosi ilikuwa siku ya mwisho kwa wagombea, vyama na miungano ya kisisasa kufanya mikutano ya kampeni kote nchini.

"Nawahakikishia Wakenya kwamba nitakuwa mwaminifu iwapo mtanichagua siku ya Jumanne. Sitakuwa mtu wa kulipiza kisasi kwa sababu katika safari yangu yote, nimekuwa na imani na maridhiano. Nitanyoosha mkono wa maridhiano iwapo nitashinda, na hata iwapo nitashindwa," alisema Odinga ambaye aliandamana na mkewe, Ida Odinga,

Aliwashukuru Wakenya kwa "kusimama na mimi katika safari yangu ya ukombozi wa nchi hii" na kumshukuru Rais Uhuru Kenyatta "kwa kuonyesha utaifa na kukumbatia maridhiano."

Ruto alipigia upatu mfumo wake wa "Bottoms Up" akisema kuwa mfumo wa ndio utakaoleta suluhisho la kudumu kwa matatizo ya kiuchumi yanayolikablili taifa hilo la Afrika Mashariki.

Alimhakikisha rais Kenyatta kwamba ataendelea kuimarish miradi aliyoanzisha na kumtaka asiwe na wasiwasi hata kama yeye (Ruto) atafanya bora zaidi endapo atachaguliwa rais.

"Hata kama uliamua kuchukua barababara nyingine na kumUunga mkono mgombea mwingine, mimi sina shida na wewe," alisema.

Ruto alisema iwapo ataunda serikali, itakuwa ni ya Wakenya wote pasina kujali kabila wala dini.

"Tunawza kunywa chai pamoja na mpinzani wangu mkuu baada ya uchaguzi wa Jumanne, lakini sitakubali kufanya mambo ya yaliyofanywa mika mitano iliyopita ya kuchanganya serikali na upinzani," alisema Ruto.

Katika hotuba zao zilizopeperushwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini, viongozi hao wawili waliwarai Wakenya kujitokeza kwa wingi ili kushiriki zoezi la kupiga kura siku ya Jumanne.

Wakenya wanajiandaa kwa uchaguzi huo unaotajwa na wachambuzi kama ambao huenda ukawa na ushindani mkali huku mirengo yote milwili ikidai kuwa ina uungwaji mkono mkubwa kote nchini.

Baadhi ya mataifa ya magaharibi tayari yametoa tahadhari kwa raia wake yakihofia kwamba huenda vurugu na ghasia zikazuka hususan katika maeneo ambayo wagombea hao wawili wana ufuasi mkubwa.

Tariban watu milioni 22 wamsajiliwa kama wapiga kura na wanatarajiwa kumchagua rais, naibu wake, magavana, maseneta, wabunge, wawakilishi wa kina mama na wawakilishi wa wadi.

Mbali na Odinga na Ruto, wagombea wengine wa urasia ni George Wajackoya wa chama cha Roots na David Mwaure Waihiga wa chama cha Agano.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka, IEBC, amenukuliwa mara kwa mara ikisema kwamba wakao tayari kuandaa uchaguzi huru na wa haki licha ya kukosolewa mara kwa mara na baadhi ya wadau.

Ruto amekuwa akilalamika kwamba utawala wa Rais Kenyatta unatumia vifaa na maafisa wa serikali kuwafnyia kampeni wanasiasa wa mrengo wa Azimio la Umoja One Kenya.

Hata hivyo, waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i amekanusha tuhuma hizo.

XS
SM
MD
LG