Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 15:38

Raila Odinga akutana na viongozi wa Ivory Coast


Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga.

Viongozi wa Afrika wanaendelea na juhudi za kidiplomasia ili kupata suluhisho la amani kwa mzozo wa kisiasa wa Ivory Coast wakati walinda amani wa umoja wa mataifa wakitafuta kuchunguza kile kinachoshukiwa kuwa ukikukaji wa haki za binadamu.

Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga anaungana na marais wa Benin Sierra, Leone na Cape Verde jumatatu kwa mazungumzo na rais aliyeko madarakani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo.

Bw. Odinga ni msuluhishi wa umoja wa Afrika kwa mzozo wa Ivory Coast ambao umeongezeka baada ya uchaguzi wa duru ya pili mwezi Novemba ambao Alassane Ouattara alidai kuwa mshindi.

XS
SM
MD
LG