Upatikanaji viungo

Raila Odinga asema al-Shabab ni kundi hatari


Waziri Mkuu wa zamani nchini Kenya, Raila Odinga
Waziri Mkuu wa zamani nchini Kenya, Raila Odinga alisema jumatano kuwa kundi la wanamgambo wa Somalia la al-Shabab ni hatari na ndio maana wakati alipokuwa madarakani akishirikiana na uongozi wa Rais Mwai Kibaki walichukua uamuzi wa kupeleka majeshi ya Kenya nchini Somalia ili kukabiliana na kundi hilo.


Bwana odinga aliyasema hayo katika mahojiano na Sauti ya Amerika-VOA- mjini Washington DC ambapo pia alizungumzia masuala mengine ya kisiasa yanayohusiana na kesi zinazomkabili Rais wa Kenya uhuru Kenyatta pamoja na naibu wake William Rutto.

Odinga alikanusha hisia zinazotolewa na baadhi ya wa-Afrika kuwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC yenye makao yake mjini The Hague inawalenga viongozi wa Afrika pekee. Alitetea utendaji kazi wa mahakama hiyo kwa kufafanua kuwa mahakama inamshitaki mtu na sio nchi inayoshitakiwa.
XS
SM
MD
LG