Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:02

Raia wawili wa DRC wahukumiwa kifungo kwa kuhusika kusafirisha bidhaa za wanyamapori


Magamba ya Kakakuona yaliokamatwa yakionyeshwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ofisi ya Forodha huko Sepang, Malaysia Mei 8, 2017. Raia wa DRC, walihukumiwa kifungo kwa kuhusika kusafirisha bidhaa za wanyamapori kutoka DRC hadi Seattle Marekani.
Magamba ya Kakakuona yaliokamatwa yakionyeshwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ofisi ya Forodha huko Sepang, Malaysia Mei 8, 2017. Raia wa DRC, walihukumiwa kifungo kwa kuhusika kusafirisha bidhaa za wanyamapori kutoka DRC hadi Seattle Marekani.

Jaji wa serikali kuu ya Marekani Jumanne aliwahukumu Herdade Lokua, miaka 34, na Jospin Mujangi, miaka 32, wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kifungo kwa kuhusika kwao kusafirisha bidhaa za wanyamapori kutoka DRC hadi Seattle Marekani.

Lokua alihukumiwa kifungo cha miezi 20 jela na Mujangi alihukumiwa kifungo cha miezi 14 jela. Wote wawili walikiri mashtaka ya kula njama na kuvunja Sheria inyofahmika kama ya Lacey, Julai 13.

Mahakama iliamua kwamba Lokua ndiye mratibu wa operesheni hiyo ya ulanguzi iliyohusisha zaidi ya washirika wengine watano ambao lengo lilikuwa kusafirisha kontena la mizigo lililojaa pembe za ndovu, pembe za faru mweupe na magamba ya Kakakuona hadi Seattle. Mujangi alisaidia kufunga bidhaa za wanyamapori na kushughulikia maelezo ya kifedha kushughulikia malipo kupitia benki ya China na kisha kurudi DRC.

Hukumu ya leo inaonyesha kwamba usafirishaji haramu wa wanyamapori utakupeleka jela, na kwamba tumejitolea kushitaki uhalifu huu," alisema Msaidizi wa Mwanasheria Mkuu Todd Kim wa Idara ya Mazingira na Maliasili wa wizara ya sheria. "Ninapongeza Uchunguzi wetu wa idara ya Usalama wa ndani na washirika wa DRC katika kukomesha biashara hii kabla ya tani ya bidhaa za wanyamapori wanaolindwa kuingia katika soko haramu.

XS
SM
MD
LG