Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 22:52

Raia wanne wa Thailand washitakiwa kwa usafirishaji haramu wa watu


Raia wanne wa Thailand wameshitakiwa Ijumaa chini ya sheria za Malaysia dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu baada ya kugundulika kwa makaburi ya halaiki ya Waislamu wa Rohingya na Bangladesh mwaka 2015 yaliyokuwa kwenye kambi katika eneo la msitu wa milima kwenye mpaka wa nchi hiyo na Thailand.

Waziri wa mambo ya ndani Saifuddin Nasution, amesema katika taarifa yake kwamba wanne hao ni miongoni mwa raia 10 wa Thailand ambao serikali iliwataka kurejeshwa mwaka 2017 kutokana na mkasa wa Wang Kelian kaskazini mwa jimbo la Perlis ambao umelishtua taifa hilo.

Kufuatia ushirikiano na serekali ya Thailand, alisema watu hao wanne walikamatwa na kurejeshwa Malaysia, Alhamisi kujibu mashtaka.

Mwezi Mei 2015, polisi wa Malaysia walitangaza kugundua kambi za msituni zilizotelekezwa zinazotumiwa na walanguzi wa binadamu wa Wang Kelian na baadaye kutoa miili 139 kutoka kwenye makaburi ya halaiki.

Forum

XS
SM
MD
LG