Kura hiyo ya maoni inajiri mwaka mmoja baada ya Saied kuivunja serikali na kulisimamisha bunge, hatua ya kujipa mamlaka zaidi ambayo wapinzani wake waliilaani na kuitaja kuwa mapinduzi ya kijeshi.
Hata hivyo, hatua ya Saied ilipongezwa na Watunisia wengi ambao walichoshwa na mdororo wa uchumi, mzozo wa kisiasa na mfumo ambao ulileta mabadiliko madogo tangu kuondolewa madarakani kwa kiongozi dikteta Zine El Abidine Ben Ali mwaka wa 2011.
Wadadisi wengi wanaamini katiba mpya itapitishwa, lakini idadi ya walioshiriki kura hiyo ya maoni itakuwa kama kipimo cha umaarufu wa Saied baada ya mwaka mmoja wa utawala unaosimamiwa na mtu mmoja ambao umeshuhudia maendeleo madogo kwa kukabiliana na matatizo ya kiuchumi katika taifa hilo la Afrika kaskazini.
Kundi linalofuatilia uchaguzi, Atide limesema katika taarifa kwamba hapakuwepo waakilishi wa kampeni za kupiga kura ya ndio au apana, na kulikuwa idadi ndogo sana ya wafualitiaji kwenye vituo vya kupigia kura.
Matokeo ya awali yanatarajiwa Jumanne alasiri majira ya huko.