Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 10:29

Raia wa Russia waliotekwa nyara nchini Niger wazungumza kupitia JNIM


Nchi ya Niger na maeneo jirani yanayopakana nao.
Nchi ya Niger na maeneo jirani yanayopakana nao.

Wawili hao walijitambulisha kuwa raia wa Russia na walisema kuwa walishikiliwa mateka huko Mbanga

Mshirika wa al-Qaeda katika ukanda wa Sahel huko Afrika Magharibi umewateka nyara raia wawili wa Russia nchini Niger, Kwa mujibu wa video iliyotolewa na kundi hilo siku ya Ijumaa.

Video kutoka taasisi ya vyombo vya habari ya Jama'a Nusrat al-Islam wa al-Muslimin (JNIM) inajumuisha kile kinachoonekana kuwa taarifa zilizochukuliwa kwenye kamera kutoka kwa watuhumiwa wawili ambao wanasema walikuwa wakifanya kazi kn kampuni moja ya Russia huko kusini magharibi mwa Niger wakati walipochukuliwa kama wafungwa.

Wakizungumza kiingereza chenye lafudhi ya Russia, wote wawili walijitambulisha kuwa raia wa Russia na walisema kuwa walishikiliwa mateka huko Mbanga, eneo la kilomita 60 magharibi mwa mji mkuu Niamey. Hawakusema ni lini tukio hilo lilitokea.

Forum

XS
SM
MD
LG