Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 07:00

Raia wa Marekani afunguliwa mashtaka ya ugaidi New York


Mahakama ya New York imefungua mashtaka dhidi ya Maalik Alim Jones
Mahakama ya New York imefungua mashtaka dhidi ya Maalik Alim Jones

Mahakama moja ya Marekani imemfungulia mashtaka raia wa Marekani mwenye miaka 31 kwa kutoa msaada wa vifaa kwa kundi la ugaidi la al-Shabab, kundi lenye msimamo mkali lenye uhusiano na al-Qaida linaloendesha harakati zake kusini mwa Somalia na eneo la maziwa makuu barani Afrika.

Mwanasheria wa Marekani, Preet Bharara katika taarifa ya Jumatatu, alimtaja mshukiwa Maalik Alim Jones mkazi wa jimbo la Maryland, nchini Marekani akishutumiwa kusafiri kwenda Somalia kwa ajili ya mafunzo kutoka kundi la al-Shabab kabla ya kubeba silaha kama mpiganaji wa ugaidi kwa taasisi ambayo imetangaza kuilenga Marekani.

Wafuasi wa kundi la Al-Shabab la nchini Somalia
Wafuasi wa kundi la Al-Shabab la nchini Somalia

Maafisa walisema Jones alisafiri kutoka Somalia kwenda New York na Kenya kupitia Morocco na umoja wa falme za kiarabu, mahala ambapo wanamshutumu alipewa mafunzo ya kuuwa na kuangamiza jamii.

Nchini Kenya, maafisa wa Marekani walisema mshukiwa alipatiwa mafunzo ya silaha za kisasa na maguruneti yanayorushwa kwa roketi za vita.

XS
SM
MD
LG