Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 27, 2025 Local time: 05:46

Raia wa Malaysia waandamana


Wanaharakati wa Malaysia wakiandamana nje ya makao ya bunge Aprili 9, 2012
Wanaharakati wa Malaysia wakiandamana nje ya makao ya bunge Aprili 9, 2012

Maelfu ya waandamanaji wakusanyika Kuala Lumpur

Polisi nchini Malaysia wamefyatua gesi ya kutoa machozi kutawanya maelfu ya waandamanaji waliokusanyika katika mji mkuu Kuala Lumpur Jumamosi wakitaka mabadiliko ya kiutawala nchini mwao. Inakisiwa watu elfu 25 walipitia kwenye vizuizi vya seng’ng’e na kuingia katika uwanja wa Independence Square huku kukiwa na ulinzi mkali na hivyo kukiuka marufuku ya kufanya mkutano wa hadhara katika uwanja huo wa mji mkuu. Polisi pia waliweka vizuizi vingine kwenye mji huo lakini kiongozi wa upinzani Anwar Ibrahim akasema nia ya waandamanaji ni kukusanyika katika uwanja huo. Wanaharakati wa Malaysia wanadai kuwa tume ya uchaguzi inapendelea chama tawala cha mseto cha waziri mkuu Najib Razak ambacho kimekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50. Aidha wanaharakati hao wanasema chama hicho kitakuwa na nafasi nzuri kushinda tena uchaguzi unaotegemea kufanyika mapema mwezi Juni.

XS
SM
MD
LG