Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 13:42

Raia wa Liberia waandamana kupinga hali ngumu ya uchumi


Maandamano ya raia wa Liberia
Maandamano ya raia wa Liberia

Maandamano makubwa yamekuwa yakijitokeza tangu rais huyo alipoingia madarakani takriban miaka mitano na hasira imezuka jinsi serikali yake inavyuoshughulikia suala la uchumi nchini , huku kukiwa na ongezeko la bei ya vyakula na mafuta likihusishwa na vita ya Ukraine na changamoto za janga la Covid 19.

Maandamano ya Jumamosi katika mji wa Monrovia kwenye wilaya ya Paynesville yaliandaliwa na umoja wa vyama vikubwa vinne vya upinzani . waandamanaji wengi walivalia mashati yaliyochapishwa sura ya Alexander Cummings ambaye ni mpizani mkubwa wa Weah katika kinyang’anyiro cha urais kwa tiketi ya ANC mwaka 2023.

Wengine walishika mabango yaliyoandikwa “ tumechoka na mateso”. Weah amekuwa nje ya nchi tangu mwishoni mwa Octoba wakati huo alitembelea Qatar kumwona mwanae wa kiume Timoth Weah akichezea timu ya Marekani katika mashindano ya kombe la Dunia na kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa Afrika na Marekani mjini Washington.

Anatarajiwa kurejea Jumatatu. Wanasiasa na wananchi wa kawaida wamelaumu kwamba wananchi wengi wanataabika hawawezi kulipa chakula, kodi ya nyumba na gharama nyingine za msingi kwa sababu ya uchumi mbovu.

XS
SM
MD
LG