Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 20:54

Raia wa DRC wapiga kura Jumatatu


Raia wa DRC wapiga kura Jumatatu

Maafisa wa tume ya uchaguzi wasema asili mia 99 ya watu nchini humo wapo tayari kushiriki katika uchaguzi

Maafisa wa tume ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanasema asili mia 99 ya watu nchini humo wapo tayari kushiriki katika uchaguzi wa urais na wabunge leo Jumatatu. Rais wa tume ya uchaguzi Daniel Ngoy - Mulunda anasema wafanyikazi wapatao 63,000 wamo kwenye vituo vya kupigia kura tayari kusaidia wapiga kura kuendeleza demokrasia nchini humo. Bwana Mulunda anasema tume ya uchaguzi inawakaribisha wakongo wote kupiga kura zao kwa amani, utulivu na heshima. Amewaomba watumie haki waliyo nayo kikatiba kuchagua rais na wabunge. Na licha ya kucheleweshwa kwa baadhi ya vifaa vya uchaguzi katika taifa hilo kubwa la Afrika ya Kati, uchaguzi wa leo Jumatatu utafanyika kama ilivyopangwa.

XS
SM
MD
LG