Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 08:26

Raia wa Afrika kusini wakabiliwa na ukosefu wa umeme.


FILE PHOTO: Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa , pichani katikati kwenye mkutano .
FILE PHOTO: Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa , pichani katikati kwenye mkutano .

Raia wa afrika kusini wamebaki katika giza kutokana na kukosekana umeme kwenye makazi ya watu na biashara kote nchini humo.

Tatizo la kukatika umeme limeshuhudiwa kwa miaka kadhaa sasa lakini wiki hii shirika la umeme nchini humo Eskom linalomilikiwa na serikali iliongeza muda na baadhi ya wakaazi na wafanyabiashara wamekosa umeme kwa zaidi ya saa tisa.

Mgomo wa wafanyakazi wa Eskom umeongeza kadhia ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na kuharibika mitambo yake iliyochakaa inayotumia makaa ya mawe . Uwezo mdogo wa kuzalisha umeme na rushwa navyo vimechangia, wanasema hayo wachambuzi wa mambo.

Hata hivyo hali hii ya kukatika umeme imejitokeza wakati ambapo Afrika kusini iko kwenye kipindi cha baridi katika ukanda wa kusini ambapo nyumba nyingi zinategemea umeme kwa ajili ya joto , mwanga na kupikia.

Biashara ndogo na kubwa zimelazimika kufungwa kwa muda mrefu au kutumia pesa nyingi kwa ajili ya mafuta ya dizeli kuendesha jenereta .

Hasira na kufadhaika kumeenea miongoni mwa wafanyabaisara na wateja kwa sababu ya ukosefu wa umeme . wataalamu wanasema tatizio hilo la umeme litakuwepo kwa muda wa miaka mingi wakati nchi ikitafuta njia za kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa Afrika kusini wa kuzalisha nishati.

XS
SM
MD
LG