Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:49

Raia mzungu wa Afrika Kusini ampiga risasi mwanamke mweusi akidai alidhani ni kiboko


ramai ya Afrika Kusini
ramai ya Afrika Kusini

Raia mzungu wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 77, ambaye ni mmiliki wa shamba, amefikishwa mahakamani Alhamisi kwa kumpiga risasi na kumjeruhi mwanamke mweusi akidai kuwa alidhani mwanamke huyo ni kiboko, polisi wamesema.

Paul Hendrik van Zyl, alikamatwa Jumanne baada ya kufyatua risasi akizielekeza kwa mwanamke huyo ambaye alikuwa anavua samaki na mpenzi wake katika mto katika mji wa Lephalale, kaskazini mwa jimbo la Limpopo.

Anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuua, kwa mujibu wa mamlaka ya kitaifa ya mashtaka ( NPA).

“Mshukiwa aliyekamatwa alidai alifyatulia risasi mnyama(kiboko), msemaji wa polisi Mamphaswa Seabi amesema katika taarifa.

Ramakone Linah mwenye umri wa miaka 38 alipata majeraha ya risasi kwenye mkono wake, naye mpenzi wake “alifanikiwa kujificha”, polisi wamesema.

Hendrik aliachiliwa kwa dhamana ya randi 1,000 sawa na dola 62 na kesi iliahirishwa kwa uchunguzi zaidi hadi tarehe 18 Mei.

Kundi la wafuasi wa chama cha upinzani chenye siasa kali za mrengo wa kushoto (EFF) chake Julius Malema, walifanya maandamano nje ya mahakama kupinga mshukiwa kuachiliwa kwa dhamana, kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na chama hicho kwenye ukurusa wa Twitter.

XS
SM
MD
LG