Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 10:58

Raia 1,400 wa Niger waondolewa kutoka Misrata


Mashambulizi katika eno la Misrata Libya.
Mashambulizi katika eno la Misrata Libya.

Afisa mwendeshaji operesheni wa msalaba mwekundu, Javier Cepero Garcia, anasema watu waliookolewa walikuwa wakiishi bila makazi ya kweli au nyumba safi kwa wiki kadhaa.

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limewaokoa takribani raia 1,400 wa Niger kutoka mji wa Misrata ulioharibiwa na vita nchini Libya.

Taarifa ya msalaba mwekundu inasema waliookolewa, wote ni raia ambao waliokolewa kati ya April 18 na 26 na walichukuliwa kwa boti kuelekea miji ya Tobruk na Benghazi, huko mashariki mwa Libya.

Afisa mwendeshaji operesheni wa msalaba mwekundu, Javier Cepero Garcia, anasema watu waliookolewa walikuwa wakiishi bila makazi ya kweli au nyumba safi kwa wiki kadhaa. Taarifa inasema uokozi umefanywa kwa uangalizi wa taasisi ya kimataifa ya masuala ya uhamiaji, ambayo inasema itawasaidia kurudi Niger kupitia Misri kama wanataka kufanya hivyo.

XS
SM
MD
LG