Hilo limetokea wakati wa shambulizi kwenye shamba moja katika kijiji cha Barire sehemu za kusini mwa nchi hiyo.
Naibu Gavana wa Lower Shabelle, Ali Nur Mohamed ameiambia VOA kwamba operesheni ilifanywa na watu wenye uhusiano na kampuni moja binafsi ya ulinzi ya Bancroft.
Kampuni hiyo inatoa mikakati na mafunzo kwa AMISOM, ofisi za Umoja wa Afrika huko Somalia ambazo zinaisaidia serikali ya nchi hiyo kupambana na kundi la wanamgambo wa al-Shabaab.
Vikosi vya nje pamoja na vichache vya Somalia vimeshambulia shamba na kuwauwa watu tisa wakiwemo watoto wadogo na watu wazima, alisema akiongeza kwamba mtu wa 10 alikufa akiwa njiani kupelekwa hospitali.
Waziri wa ulinzi, Abdirashid Mohamed Abdullahi alikanusha kwamba kampuni binafsi ya ulinzi ya Bancroft ilihusika.