Watu wapatao 16 waliuwawa na wengine kadhaa walijeruhiwa baada ya radi kupiga kwenye jengo la kanisa moja la Sabato katika wilaya ya Nyaruguru huko Rwanda.
Nchi ya Rwanda kwa sasa inashuhudia kipindi cha msimu za mvua za hapa na pale lakini kulingana na mwandishi wa Sauti ya Amerika-VOA mjini Kigali, Silvanus Karemera, hakuna onyo la aina yeyote kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ambalo lilitolewa kwa siku ya Jumamosi kutoka idara inayohusika na hali ya hewa nchini humo ili kusaidia watu na jamii kwa jumla kuweza kuchukua tahadhari.