Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 03:07

Qatar yatingwa 2-0 na Equador katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia


FIFA Kombe la Dunia Qatar 2022 - Grupu A - Qatar v Ecuador
FIFA Kombe la Dunia Qatar 2022 - Grupu A - Qatar v Ecuador

Ecuador waliwashinda Qatar ambao walikuwa wanacheza kwa mara ya kwanza katika  michuano ya kombe la dunia, kwa mabao mawili kwa sufuri Jumapili, ambayo yalipachikwa na mshambuliaji mkongwe Enner Valencia, katika siku ambayo hafla ya ufunguzi rasmi wa mashindano hayo ya mwezi mmoja ilifanyika.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa taifa mwenyeji wa mashindandano hayo, kushindwa katika mechi ya ufunguzi, katika historia ya kinyang’anyiro hicho.

Mfungaji bora wa Ecuador, aliyepewa jina la utani la "Superman" akiwa nyumbani, alifunga penalti ya mapema na kuongeza bao la kichwa mnamo dakika ya 31 na kuipatia nchi hiyo ya Amerika ya Kusiani bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza huku Qatar wakionekana kuzidiwa na ukubwa wa mchezo huo.

Mechi hiyo ya kwanza ilitazamwa moja kwa moja na zaidi ya mashabiki 67,372 kwenye uwanja wa Al Bayt.

Pande zote mbili sasa zinapaswa kucheza na Senegal na Uholanzi katika hatua ya makundi, huku nafasi ya Qatar kuchukua pointi, au kufuzu ikionekana kuwa ndogo kwenye kiwango hicho.

XS
SM
MD
LG