Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 15:15

Qatar yaondoa maelfu ya wafanyakazi wa kigeni katika nyumba katikati ya Doha


Muonekano wa jumla wa anga ya Doha. REUTERS
Muonekano wa jumla wa anga ya Doha. REUTERS

Qatar imewaondoa  maelfu ya wafanyakazi wa kigeni waliokuwa wanaishi katika nyumba  katika maeneo ya  katikati mwa mji mkuu wa Doha ambapo mashabiki wa soka wanaozuru nchi hiyo wanatarajiwa kukaa wakati wa Kombe la Dunia, wafanyakazi hao waliofukuzwa kutoka kwenye  nyumba zao waliiambia Reuters.

Walisema kwamba zaidi ya majengo kumi na mbili watu wameondolewa na nyumba hizo kufungwa na mamlaka, na kuwalazimisha wafanyakazi hasa Waasia na Waafrika kutafuta makazi wanayoweza kupata ikiwa ni pamoja na kulala barabarani nje ya nyumba zao za zamani.

Hatua hiyo imekuja chini ya wiki nne kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ya soka ya kimataifa hapo Novemba 20 ambayo imeibua uchunguzi wa kina wa kimataifa kuhusu jinsi Qatar inavyowatendea wafanyakazi wa kigeni na sheria zake za ustawi wa jamii zenye vikwazo.

Katika jengo moja ambalo wakaazi walisema lilikuwa na watu 1,200 katika wilaya ya Al Mansoura mjini Doha, viongozi waliwaambia watu mnamo saa nane mchana siku ya Jumatano kwamba walikuwa na saa mbili tu kuondoka kwenye makazi yao.

Maafisa wa manispaa walirejea mwendo wa saa nne ne nusu usiku na kuwalazimisha watu wote kutoka nje na kufunga milango ya jengo hilo, walisema. Watu wengine hawakuweza kurudi kwa wakati kukusanya mali zao.

“Hatuna mahali popote pa kwenda," mtu mmoja aliiambia Reuters siku iliyofuata alipokuwa akijiandaa kulala nje kwa usiku wa pili na wanaume wengine wapatao 10, baadhi yao wakiwa hawana mashati katika joto la vuli na unyevunyevu katika taifa hilo la Ghuba ya Kiarabu.

Mtu huyo na wafanyakazi wengine wengi waliozungumza na Reuters, walikataa kutoa majina yao au maelezo yao binafsi kwa kuhofia kulipiziwa kisasi na mamlaka au waajiri wao.

Karibu na hapo, wanaume watano walikuwa wakipakia godoro na friji ndogo nyuma ya lori. Walisema wamepata chumba huko Sumaysimah, kama kilomita 40 Kaskazini mwa Doha.

Afisa wa serikali ya Qatar alisema kufukuzwa huko hakuhusiani na Kombe la Dunia na kulipangwa kulingana na mipango inayoendelea ya kina na ya muda mrefu ya kupanga upya maeneo ya Doha.

"Wote tangu wakati huo wamehamishiwa katika makazi salama na yanayofaa," afisa huyo alisema, akiongeza kwamba maombi ya kuhamishwa "yangefanywa kwa taarifa maalum."

Shirikisho la soka duniani FIFA halikujibu ombi la maoni na waandaaji wa Kombe la Dunia la Qatar walielekeza maswali kwa upande wa serikali.

“Ghetto la Makusudi"

Kiasi cha asilimia 85 ya idadi ya watu milioni 3 nchini Watar ni wafnayakazi wa kigeni. Wengi wao walioondolewa makazini ni madereva, vibarua au wenye kandarasi na makampuni lakini wanahusika na kujitafutia makazi yao wenyewe – kinyume na makampuni makubwa ya ujenzi ambao wafanyakazi wanaishi katika nyumba maalum ambazo zinahudumia maelfu ya watu.
Mfanyakazi mmoja alisema kufukuzwa kwenye nyumba kuliwalenga wanaume wasiokuwa na wake, wakati wafanyakazi wa kigeni wenye familia hawakuathiriwa.
Mwandishi wa Reuters aliona zadi ya dazeni ya majengo ambako wakazi walisema watu wameondolewa. Baadhiya majengo yalikatiwa umeme.

Majengo mengi yalikuwa kwenye ujirani ambako serikali imekodisha majengo kwa ajili ya kutoa makazi kwa mashabiki wa Kombe la Dunia. Tovuti ya waandaaji imeorodhesha majengo huko Al Mansoura na wilaya nyingineambako majengo yametangazwa kukodishwa kati ya dola 240 na 426 kwa usiku mmoja.

Afisa wa Qatar alisema mamlaka ya manispaa imekuwa ikiimarisha tangy mwaka 2010 sheria ya Qatar ambayo inapiga marufuku ‘wafanyakazi’ kuishi ndani ya maeneo ya makazi yenye familia – eneo ambalo limetajwa ni katikati ya Doha – na imepewa mamlaka ya kuwahamisha watu.

Baadhi ya wafanyakazi walioondolewa walisema walikuwa na matumaini ya kutafuta sehemu za kuishi huku kukiwa na mpango wa uejnzi wa makazi ya wafanyakazi ndani na kuzunguka eneo la viwanda katika viunga vya kusini maghairbi mwa Doha au katika miji iliiyo nje kidogo ambapo usafiri wa kwenda kazini utachukua muda mrefu.

Kuwafukuza wafanyakazi “kunaiweka Qatar katika hali ya kupendeza na kifahari bila ya kukiri kwamba wafanyakazi wanaolipwa ujira wa chini ndiyo wamefanya iwezekane,” alisema Vani Saraswathi, Mkuruguenzi wa Miradi katika Migrant-Rights.org, ambayo inawatetea wafanyakazi wageni huko Mashariki ya Kati.

Baadhi ya wafanyakazi wamesema walikumbana na hali hii ya kufukuzwa hapo kabla.

MMoja alisema alilazimishwa kubadili majengo huko Al Mansoura mwishoni mwa mwezi Septemba halafu kutolewa tena siku 11 baadaye bila ya notisi ya mapema, pamoja na wenzeka wengine. “Katika dakika mojka, tulilazimika kuhama,” alisema.

Mohamed dereva kutoka Bangladesh, alisema aliishi katika ujirani huo kwa miaka 14 mpaka Jumatano, wakati manispaa ilipomueleza ana saza 48 kuondoka katika nyumba aliyokuwa akiishi pamoja na wenzake wengine 38.

Alisema vibarua ambao walijenga miundo mbinu kwa Qatar ili kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia walisukumwa pembeni wakati mashindano yanakaribia.

“Nani amejenga viwanja vya mpira? Nani alijenga barabara? Nani alijenga kila kitu? Wabengali, wapakistan. Watu kama sisi. Hivi sasa wanatuondoa sote twende nje.

XS
SM
MD
LG