Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 20:12

Qatar imekasirishwa na shutuma za kila mara 'kwa kuandaa' kombe la dunia


Watalii wakiwa mbele ya maandishi yaliyojengwa kutangaza maandalizi ya mashindano ya mpira ya kombe la dunia, Doha, Oct 23, 2022
Watalii wakiwa mbele ya maandishi yaliyojengwa kutangaza maandalizi ya mashindano ya mpira ya kombe la dunia, Doha, Oct 23, 2022

Mtawala wa Qatar ameelezea kughadhabishwa na ukosoaji unaoendelea kuhusiana na taifa hilo la kwanza la kiarabu kuwa mwenyeji wa mashindano ya kandanda kombe la dunia mwaka huu 2022.

Qatar imeshutumiwa kwa kile kilichotajwa kama ukandamizaji wa wahamiaji na watu walio katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja, tangu iliposhinda haki ya kuandaa mashindani ya kandanda ya kombe la dunia.

Katika hotuba kwa bunge la Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, amesema kwamba Qatar imekabiliana na shutuma zisizo za msingi ambazo hakuna nchi nyingine iliyowahi kuandaa kombe la dunia imekabiliana nazo.

"Awali, tulikabiliana na swala hili kwa nia njema na hata kuchukulia baadhi ya ukosoaji kwa nia nzuria kabisa na kwa mtazamo kwamba ukosoaji huo ulikuwa muhimu kwa kujijenga wenyewe. Lakini sasa imekuwa Dhahiri kwamba kampeni hiyo inaendelea na kupanuka zaidi na kuwa uongo na misimamo mikali na kupelekea watu wengi kuanza kuuliza sababu mahsusi zinazopelekea kampeni hiyo kufanyika," amesema Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani

Madai ya ukandamizaji wahamiaji ikiwemo malipo duni kwa wafanyakazi wanaochangia katika uchumi wa Qatar kukua kwa haraka, na kujenga viwanja vya michezo, yamekuwa yakitolewa kila mara na kupelekea maandamano kote duniani hasa Ulaya.

Qatar imekuwa ikikanusha madai hayo na kusisitiza kwamba imeimarisha ulinzi kwa wahamiaji na kwamba ukosoaji huo hauna msingi wowote.

Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yameisifia Qatar kwa kuboresha sheria zake za kazi na kuweka nyongeza ya mshahara kufikia dola 275 kila mwezi, kufikia mwaka 2020, pamoja na kuondoa mfumo uliokuwa unawazuia wafanyakazi kubadilisha kazi au kuondoka nchini bila ruhusa ya waajiri wao.

XS
SM
MD
LG