Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:07

Putin: Russia  inataka kukomesha vita nchini Ukraine


 Vladimir Putin alipokutana na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan mjini Vladivostok. Septembea 7, 2022. Valery Sharifulin
Vladimir Putin alipokutana na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan mjini Vladivostok. Septembea 7, 2022. Valery Sharifulin

Rais wa Russia Vladimir Putin alisema siku ya Alhamisi kwamba Russia inataka kukomesha vita nchini Ukraine na kwamba bila shaka hilo litahusisha suluhu ya kidiplomasia.

Putin alitoa maoni hayo siku moja baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kumkaribisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy katika Ikulu ya Marekani na kumuahidi kuendelea kumuunga mkono bila kutetereka.

“Lengo letu sio kuzungusha gurudumu la mzozo wa kijeshi, lakini, kinyume na hivyo, kumaliza vita hivi," Putin alisema. "Tutajitahidi kulimaliza hili, mapema iwezekanavyo itakuwa bora zaidi, bila shaka."

Msemaji wa Ikulu ya Marekani John Kirby alisema Putin "hajaonyesha dalili zozote kwamba yuko tayari kufanya mazungumzo" ya kukomesha vita, vilivyoanza wakati Moscow ilipotuma wanajeshi nchini Ukraine Februari 24.

Kinyume kabisa na hivyo," Kirby aliwaambia waandishi wa habari wakati wa mkutano wa mtandaoni. "Kila kitu anachofanya (Putin) ardhini na angani kinaonyesha mtu ambaye anataka kuendelea kuwadhuru watu wa Ukraine" na "kuzidisha vita."

XS
SM
MD
LG