Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 03:20

Russia:Putin atofautiana na Rais Medvedev juu ya Libya


Rais wa Russia, Dmitry Medvedev akizungumza na waandishi wa habari kwenye makazi yake huko Gorki nje ya Moscow, March 21, 2011
Rais wa Russia, Dmitry Medvedev akizungumza na waandishi wa habari kwenye makazi yake huko Gorki nje ya Moscow, March 21, 2011

Katika tukio lisilo la kawaida la mgawanyiko baina ya viongozi wakuu wa Russia, Rais wa Russia Dmitry Medvedev amesema matamshi ya waziri mkuu wa nchi hiyo, Vladmir Putin juu ya Libya, hayakubaliki.

Mwandishi wa VOA James Brooke anaripoti kutoka Moscow kuwa viongozi hao wakuu wa Russia wamekuwa na migawanyiko ambayo hufichwa mbele ya umma. Bwana Putin akitizama upande wa Magharibi, Medvedev hutizama upande wa Mashariki. Kwa zaidi ya miaka mitatu, viongozi hawa wawili wamejaribu kuficha tofauti zao, lakini sasa hali ya wasiwasi kwa umma juu ya Libya ni dhahiri.

Bwana Putin akizuru katika kiwanda cha kijeshi cha silaha, alilaani azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lililoruhusu hatua ya kijeshi dhidi ya vikosi vya Ghadafi.

Mataifa yaliyopeleka ndege zake za kivita kupambana na Ghadafi ni pamoja na Uingereza, Ufaransa na Italy.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rais Medvedev wa Russia alisema haikubaliki kamwe kutumia maneno yanayozozana na ustaarabu wa nchi nyingine, akiashiria tamko la Waziri Mkuu, Putin kupinga hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya utawala wa Ghadafi.

Hata hivyo Rais huyo alitetea uamuzi wa Russia wa kutounga mkono azimio hilo, akisema lilikuwa na dosari kiasi ingawa haamini kwamba azimio lenyewe lina makosa makubwa. Hapo awali bwana Putin, alikuwa amesema azimio hilo limejaa kasoro na makosa.

Akiwa kwenye ziara yake katika kiwanda hicho cha silaha za kijeshi kilichopo katikati ya Russia, bwana Putin, alielezea zaidi juu ya sera zake za kigeni. Alionya kuwa sera za Marekani zimeendelea kuwa za mwendo uliopo, akiashiria mashambulizi ya angani ya Marekani dhidi ya Belgrade, vita vya Iraq na Afghanistan na kusema sasa Marekani imegeukia Libya, ikisingizia kuwalinda raia. Putin aliendelea kuhoji, uhalali wa hatua hiyo, akisema hamna sababu yoyote ya kuvamia Libya.

Lakini Mjini Moscow Rais Medvedev alisisitiza kwa waandishi wa habari kuwa hatua ya kijeshi iliyochukuliwa na nchi za magharibi dhidi ya Libya, zinatokana na tabia mbaya na ya muda mrefu ya uongozi wa Libya kuwatendea uhalifu raia wake.


XS
SM
MD
LG