Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:24

Putin hatafanya mkutano na waandishi wa habari ilivyo kawaida yake kila mwisho wa mwaka


Rais wa Russia Vladimir Putin Nov. 9, 2022.
Rais wa Russia Vladimir Putin Nov. 9, 2022.

Rais wa Russia Vladimir Putin hatawahutubia waandishi wa habari kama ilivyo kawaida yake kila mwisho wa mwaka, ikiwa ni mara ya kwanza kutofanya hivyo katika muda wa muongo mzima.

Kwa kawaida, kikao cha Putin na waandishi wa habari huchukua saa kadhaa na kimekuwa sehemu ya shughuli za putin katika kalenda ya kila mwaka ambapo huwa anajibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari wa ndani na wa kimataifa.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov, amewaambia waandishi wa habari kwamba kikao hicho cha habari cha kufunga mwaka, hakitafanyika.

Peskov hata hivyo amesema kwamba Putin amekuwa akizungumza na waandishi wa habari kila mara, ikiwemo anapotembelewa na viongozi kutoka nchi nyingine, na kwamba kiongozi huyo wa Russia atapata fursa nyingine ya kuzungumza na waandishi wa habari.

Peskov hajasema sababu ambazo zimepelekea kikao cha mwaka huu kutofanyika.

Vita vya Russia nchini Ukraine vimeingia mwezi wa 10 na utawala wa Putin unakabiliwa na ukosoaji mkubwa kuhusiana na mkakati wake wa kivita, baada ya wanajeshi wa Russia kushindwa kuudhibithi mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv na kulazimishwa kuondoka mjini Kherson licha ya kuongeza idadi ya wanajeshi nchini Ukraine huku ikihojiwa iwapo wanajeshi waliosajiliwa walipokea mafunzo ya kutosha.

XS
SM
MD
LG