Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:39

Putin hana mipango ya kuhudhuria mazishi ya Prigozhin, Kremlin imesema


Picha ya kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigozhin imewekwa kwenye eneo la ukumbusho la barabarani lisilo rasmi karibu na ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Agosti 26, 2023.

Rais wa Russia Vladimir Putin hana mipango ya kuhudhuria mazishi ya kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin ambaye alifariki wakati ndege yake ilipoanguka wiki iliyopita, Kremlin imesema Jumanne.

Ndege binifasi ambayo Prigozhin alikuwa anasafiri nayo kuelekea St Petersburg kutoka Moscow ilianguka katika mkoa wa Tver kaskazini mwa Moscow Agosti 23 huku watu wote 10 waliokuwa ndani ya ndege hiyo walifariki, wakiwemo viongozi wawili wakuu wa Wagner na wanaume wanne walioripotiwa kuwa walinzi wa Prigozhin.

Bado haijafahamika wazi kilichosababisha ajali hiyo lakini wanakijiji waishio karibu na eneo la tukio waliliambia shirika la habari la Reuters kwamba walisikia mlipuko na kuiona ndege hiyo ikianguka chini.

Akiulizwa ikiwa Putin atahudhuria mazishi ya Prighozin, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari “Kuwepo kwa rais hakutarajiwi”.

Peskov amesema Kremlin haina taarifa yoyote maalum kuhusu mipango ya mazishi, na mipango inahusu familia yake.

Forum

XS
SM
MD
LG