Katika safari yake ya pili inayojulikana nje ya nchi tangu mahakama ya kimataifa ya uhalifu yenye makao yake The Hague kutoa hati ya kukamatwa kwake mwezi machi, Putin na msafara wake walisafiri kwa ndege hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa mji mkuu wa Beijing Jumanne asubuhi.
Alipokelewa na waziri wa biashara wa China wang Wentao.
Pia ni safari ya kwanza rasmi ya mkuu wa Kremlin nje ya uliokuwa umoja wa sovieti mwaka 2023, baada ya kuzuru Kirigizstan, Jamhuri ya zamani ya Soviet mapema mwezi huu.
ICC inamshutumu Putin kwa kuwarejesha kinyume cha sheria watoto kutoka Ukraine, hati inazitaka nchi wanachama 123 wa Mahakama hiyo kumkamata Putin na kumpeleka The Hague kwa ajili ya kusomewa mashtaka iwapo atakanyaga katika ardhi yao.
Si Kirigizstan wala China ni wanachama wa ICC iliyoanzishwa ili kusimamia na kuendesha kesi za uhalifu wa kivita.
Forum