Putin atagombea muhula wa tano wa Kremlin, katika uchaguzi usio na upinzani wa kweli ambao utafanyika ikiwa ni zaidi ya miaka miwili tangu aanzishe mashambulizi ya uvamizi wa Ukraine.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 71 aliingia madarakani mwaka wa 2000, na kizazi kizima cha Russia cha sasa hakikumbuki maisha bila yeye.
Kura hiyo itaongeza muda wa utawala wake mpaka 2030 na kumpa uwezekano wa kukaa Kremlin mpaka mwaka 2036.
“Lazima tukumbuke na kamwe tusisahau na kuwaambia watoto wetu, Russia, itakuwa nchi huru inayojitosheleza,” Putin amesema wakati wa kongamano la chama tawala cha United Russia.
Forum