Kumbukumbu ya kuadhimisha miaka 80 tangu kukombolewa kwa kambi ya Auschwitz, nchini Poland kulikofanywa na wanajeshi wa Sovieti, ilihudhuriwa na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, Mfalme Charles wa Uingereza, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Rais wa Poland Andrzej Duda na viongozi wengine wengi.
Russia, mrithi wa Muungano wa Sovieti, haikualikwa kutokana na vita vya Ukraine.
“Hili ni jambo la kushangaza na la aibu,” Rais Putin amesema kupitia televisheni ya serikali ya Russia, katika mahojiano yaliyorushwa Jumapili.
Forum