Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 13:50

Putin alidanganywa kuhusu vita vya Ukraine - White house


Rais wa Russia Vladimir Putin katika mojawapo ya mikutano yake mjini Moscow, March 21, 2022. Picha ya AP
Rais wa Russia Vladimir Putin katika mojawapo ya mikutano yake mjini Moscow, March 21, 2022. Picha ya AP

Ikulu ya Marekani White house, imesema kwamba rais wa Russia Vladimir Putin hakupewa habari za kweli kuhusu athari ambazo zingetokana na vita vya Ukraine, na kwamba uhusiano wake na maafisa wake umeharibika.

White house imesema hayo kwa kuzingatia taarifa za kijasusi za Marekani.

Mkuu wa mawasiliano wa white house Kate Bedingfield amesema kwamba wana taarifa za uhakika kwamba Putin anahisi kwamba hakupewa taarifa za uhakika na maafisa wake wa kijeshi.

"Tunaamini kwamba anapewa taarifa zisizo za kweli na washauri wake kuhusu namna wanajeshi wake wameshindwa katika malengo yao na namna uchumi wa Russia unavyoathirika kutokana na vikwazo, kwa sababu washauri wake wana uoga mkubwa kusema ukweli.” Amesema Kate Bedingfield.

Wanajeshi wa Ukraine wamekuwa wakidhibithi sehemu kadhaa kutoka kwa wanajeshi wa Russia, katika siku za hivi karibuni, ikiwemi mji muhimu wa Kyiv na sehemu zilizo karibu na mji huo, za Irpin.

Mashambulizi ya Russia yanaonekana kupungua nguvu, ikiwa ni mwezi mmoja tangu walipoingia nchini Ukraine, Februari 24.

Katika sehemu za Irpin, mji unaopita kabla ya kuingia Kyiv, meya Oleksandr Markushyn, amesema kwamba mashambulizi ya mabomu yanaendelea na kwamba watu kadhaa wameuawa kutokana na mashambulizi hayo ya wanajeshi wa Russia, licha ya Moscow kusema kwamba wamesitisha mashambulizi.

Katika juhudi za kidiplomasia zinazoendelea, waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu, amesema kwamba bilionea oligarch Roman Abramovich, ambaye ni raia wa Russia, na ambaye ameekewa vikwazo na nchi za Ulaya kuhusiana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine, anafanya kila juhudi kumaliza vita hivyo.

Amesema kwamba Abramovich, amekuwa akishirikiana na utawala wa Kyiv pamoja na Moscow tangu uvamizi huo ulipotokea Februari 24.

Abramovich alihudhuria mazungumzo kati ya Ukraine na Russia mjini Istanbul, jumanne wiki hii, bila mwaliko.

Cavusoglu vile vile amesema kwamba atasafiri hadi Israel na Palestina, akiandamana na waziri wa nshati Fatih Donmez, katikati ya mwezi May, kwa mazungumzo kuhusu uteuzi wa mabalozi katika nchi hizo za Israel na Palestina.

Amesema kwamba hatua ya kutaka kuacha kutegemea mafuta kutoka Russia, huenda isifanyike kwa haraka.

XS
SM
MD
LG