Amesema taifa la Ukraine kwa sasa lipo katika mtego mpya wa Unazi.
Katika hotuba yake kali huko Volgograd, iliyojulikana kama Stalingrad mpaka 1961, Putin aliilaumu Ujerumani kwa kusaidia kuipatia Ukraine silaha na kusema, sio mara ya kwanza, kwamba yuko tayari kutumia silaha nzima ya Russia, ikijumuisha silaha za nyuklia.
"Kwa bahati mbaya, tunaona itikadi ya Unazi katika mfumo wake wa kisasa na udhihirisho tena unatishia moja kwa moja usalama wa nchi yetu," Putin aliiambia hadhira ya maafisa wa jeshi na wanachama wa vikundi vya wazalendo na vya vijana.
Maafisa wa Russia wamekuwa wakilinganisha na mapambano dhidi ya Wanazi toka vikosi vya vyao vilipoingia Ukraine karibu mwaka mmoja uliopita.
Facebook Forum