Mapigano yalizuka Jumanne baina ya vikosi vya usalama vya Puntland, kitengo cha kukabiliana na ugaidi ambacho kilikuwa kinasaidiwa na Marekani, na vikosi vya kawaida vya usalama vya kikanda.
Takriban watu 14 waliuwawa na wengine 63 kujeruhiwa, kwa mujibu wa mashuhuda na vyanzo vya hospitali. Pande hizo zilijibizana kwa kufyatuliana risasi kwa kutumia bastola bunduki za rashasha na milipuko na kulazimisha wakazi kukimbia kwa mujibu wa shuhuda waliozungumza na VOA.
Waziri wa usalama wa eneo hilo Abdisamad Mohamed Galan ametangaza kusimamishwa mapigano Jumatano, akisema uamuzi huo ulifanywa baada ya viongozi wa kimila, wanazuoni, na viongozi wa kibiashara kuingilia kati.