Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 15:52

Papa Francis akemea silaha za nyuklia


Baba mtakatifu Francis

Baba mtakatifu Francis, Jumapili ametoa wito wa kupigwa marufuku silaha za nyuklia wakati Japan ikiadhimisha miaka 70 tangu Marekani ilpodondosha bomu la Atomic huko Nagasaki siku chache kabla ya kumalizika kwa vita vya pili vya dunia.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki amesema kuwa kumbukumbu ya mabomu ya Atomic huko Hiroshima na Nagasaki mapema agosti 1945 itabaki kuwa wito wa kuangamizwa kwa silaha za nyuklia.

Amesema itabaki kuwa onyo la kudumu kwa dunia kukataa vita milele na kuangamiza silaha za nyuklia na kila silaha ya uharibifu wa halaiki.

Baba mtakatifu Francis amesema kuwa angetamani kuwe na sauti moja inayosema “hapana vita”, “hapana ghasia”, lakini ndio kwa mashauriano na ndio kwa Amani.

Wakati wa mapigano, ameongeza kusema kuwa kila mmoja hupoteza.

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameweka shada la maua kwenye sherehe hizo zilizofanyika huko Nagasaki na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka mataifa 75 akiwemo balozi wa marekani Caroline Kennedy.

XS
SM
MD
LG