Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 29, 2020 Local time: 05:50

Papa Francis kutembelea Kenya na Uganda


Papa Francis ashangiliwa na waumini Vatican.

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis atatembelea Kenya Novemba 25 kabla ya kuelekea Uganda siku mbili baadaye.

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis atatembelea Kenya Novemba 25 kabla ya kuelekea Uganda siku mbili baadaye na kisha Jamhuri ya Afrika ya Kati hapo tarehe 29 mwezi huo.

Mwezi Juni kiongozi huyo mzaliwa wa Argentina alieleza kikao cha makasisi kutoka kote ulimwenguni kuwa alikusudia kufanya ziara yake ya kwanza barani Afrika kwa kutembelea Kenya ingawaje ziara hiyo haikuwa imedhibitishwa wakati huo kutokana na matatizo ya kimipango.

Papa Francis hakufafanua matatizo hayo lakini alikuwa akizungumza miezi miwili baada ya kundi la wanamgambo kutoka Somalia la Al-Shabaab kushambulia wakristo kwenye chuo kikuu karibu na mji wa Garissa ambapo wanafunzi 148 waliuwawa. Nchi ya Kenya imeshuhudia mashambulizi ya kigaidi ya mara kwa mara kutoka wanamgambo wa Al-Shaabab.

Ona maoni (2)

mjadala huu umefungwa

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG