Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 05:31

Polisi Tanzania yachunguza uvamizi nyumbani kwa mbunge


Joshua Nassari

Jeshi la Polisi mkoani Arusha, Tanzania limeanza uchunguzi wa tukio la kuvamiwa kwa Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Joshua Nassari.

Nassari alivamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake eneo la Meru Nkwaninkole na mbwa wake kupigwa risasi katika shambulio la silaha lililofanywa usiku wa kuamkia juzi na watuhumiwa kukimbilia kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kupata taarifa ya tukio hilo na kusema kuwa kazi ya uchunguzi iachiwe jeshi hilo.

Nassari, ambaye ni mbunge wa Arumeru Masharikialisema mbele ya waandishi wa habari kuwa alivamiwa na watu hao saa sita usiku baada ya kutoka kuhudhuria kongamano la vijana lililokuwa likifanyika katika Chuo cha Mafunzo na Maendeleo ya Kimataifa (MST DC) eneo la Denish.

Akisimulia tukio hilo Nassari ameeleza kuwa wakati akiwa ndani ya chumba chake amelala ghafla alisikia kelele za mbwa akibweka na alipojaribu kuchungulia alisikia mlio wa risasi na ndipo alipochukua bunduki yake na kuanza kufyatua juu kwa lengo la kujihami.

Idadi kamili ya wahalifu hao haikuweza kujulikana alisema Nassari. Kwa mujibu wa mbunge huyo alipotoka nje wahalifu hao tayari walikuwa wameruka ukuta na kutoweka waliposikia akijibu shambulio hilo kwa kutumia silaha yake ya kujilinda anayoimiliki.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG