Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 16:22

Polisi wawili wauawa Sierra Leonne katika maandamano ya kupinga hali ngumu ya uchumi


Rais wa Sierra Leonne Julius Maada Bio. Picha ya AFP
Rais wa Sierra Leonne Julius Maada Bio. Picha ya AFP

Maafisa wawili wa polisi wameuawa Jumatano nchini Sierra Leonne baada ya maandamano dhidi ya hali ngumu ya uchumi kugeuka kuwa mapambano kati ya maafisa wa usalama na vijana wanaomtaka rais ajiuluzu, polisi wamesema.

Msemaji wa polisi Brima Kamara ameiambia AFP kwamba “ maafisa wawili wa polisi, mwanaume na mwanamke, walipigwa hadi kufa mashariki mwa mji mkuu Freetown Jumatano asubuhi.”

Makamu rais Mohamed Juldeh Jalloh ametangaza amri ya kutotoka nje usiku na kusema “ Wasierra Leonne wasiokuwa na hatia wakiwemo wafanyakazi wa usalama waliuawa”.

Polisi wamesema darzeni ya waandamanaji walikamatwa.

Mfanyakazi wa afya kwenye hospitali ya Freetown amesema darzeni ya watu walijeruhiwa.

Waandamanaji wamesikika wakiimba “ Bio anapaswa kuondoka”, wakimaanisha rais Julius Maada Bio, ambaye yuko ziarani nchini Uingereza katika ziara binafasi.

Mtandao wa intaneti ulifungwa kwa muda mjini Freetown Jumatano alasiri, kwa mujibu wa tovuti ya NetBlocks, inayofuatilia mawasiliano ya intaneti.

XS
SM
MD
LG