Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 18:19

Polisi wathibitisha watu 8 wameuawa Indianapolis, Marekani

Polisi wakifanya doria katika eneo la tokio la mauaji katika jengo la FedEx huko mjini Indianapolis, Indiana, Marekani Aprili 16, 2021, Kevin Powell/Indy First Alert/via REUTERS
Polisi wakifanya doria katika eneo la tokio la mauaji katika jengo la FedEx huko mjini Indianapolis, Indiana, Marekani Aprili 16, 2021, Kevin Powell/Indy First Alert/via REUTERS

Polisi katika mji wa Indianapolis, Indiana, Marekani wanasema watu wanane wamepigwa risasi na kuuawa kwenye kituo cha FedEx.

Mshambualiaji baadaye alijiua mwenyewe. Msemaji wa polisi anasema watu kadhaa wengine walijeruhiwa jana Alhamisi usiku katika tukio hilo.

Watu wanne wamelazwa hospitali, akiwemo mtu ambaye ana majeraha mabaya.

Mtu mwingine wa pili alitibiwa kwenye eneo la tukio. Mfyatuaji risasi bado hajatambuliwa.

Polisi bado wako katika eneo la tukio kuhoji watu nyakati za alfajiri hivi leo Ijumaa.

Eneo hilo la tukio liko karibu na uwanja wa kimataifa wa ndege wa Indianapolis.

XS
SM
MD
LG