Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 22:59

Polisi watawanya maandamano Kenya


Polisi wa Kenya walirusha gesi ya kutoa machozi kwenye msafara wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga, Ijumaa wakati watu walipojiunga na maandamano dhidi ya serikali katika miji kadhaa kuhusu mgogoro mkubwa wa gharama za maisha na msururu wa ongezeko la kodi lenye utata

Mabomu ya machozi yalirushwa kwenye msafara wa Odinga, baada ya kuhutubia mkutano mkubwa katika mji mkuu Nairobi, waandishi wa AFP walisema, na polisi walichukua hatua sawa na kuvunja maandamano katika mji wa bandari Mombasa, na Kisumu, ngome ya upinzani kwenye Ziwa Victoria.

Polisi walikuwa wamejitokeza kukabiliana na maandamano yaliyoitishwa na Odinga mwaka huu kuhusu sera za serikali ya Rais William Ruto.

Katika mkutano huo, Odinga, ambaye alishindwa katika uchaguzi wa Agosti 2022 alitangaza mipango ya kukusanya sahihi milioni 10 katika jitihada za kumwondoa mpinzani wake mkuu madarakani.

Forum

XS
SM
MD
LG