Kikosi kwenye kituo cha polisi cha Sona kilikanyaga kilipuzi na kulifuatia ufyatuaji mkali wa risasi uliofanywa na washambuliaji ambao hawajajulikana”, idara ya polisi imesema katika taarifa.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa “maafisa watano wa polisi waliuawa, mmoja akajeruhiwa na wengine watatu wametoweka.”
Shambulio hilo lilifanyika katika mji wa Sona, katika eneo la Koutiala, karibu na mpaka kati ya Mali na Burkina Faso.
Afisa wa eneo hilo aliyechaguliwa na afisa mmoja wa polisi ya taifa, wote wakizungumza na AFP kwa masharti ya kutotajwa majina yao, wamewaelezea washambuliaji kuwa ni magaidi.
Mali inakabiliwa na uasi wa muda mrefu wa wanamgambo wa kiislamu ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu na kulazimisha maelfu ya wengine kuhama makazi yao.