Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 06, 2023 Local time: 00:22

Polisi watano wa Kenya wadaiwa kuuwawa


Polisi watano wa Kenya wanadaiwa kuuwawa kwa bomu la kutegwa barabarani huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu wa Idhaa ya Kiswahili mjini Mombasa, Josephat Kioko aliyeongea na maafisa wa Kenya waliokataa kutajwa majina yao, amesema tukio hilo lilitokea Jumanne katika eneo la Pwani ya Kenya.

Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo ambalo lipo karibu na mpaka wa Somalia, wamedai walisikia mashambulizi ya wahalifu wanaodaiwa kuwa ni wanachama wa kundi la Al-Shabab la Somalia na maafisa wa usalama wa Kenya.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyeongea na wakazi hao pamoja na maafisa wa Kenya, inaelezwa watu hao baada ya kufanya mashambulizi hayo walikimbilia msituni na kuacha maafa ya mauaji ya wana usalama watano wa Kenya.

XS
SM
MD
LG