Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 12:34

Watu wawili zaidi wakamatwa na polisi Uingereza


Polisi wafanya msako mkali katika eneo la Sunbury-on-Thames, England, Saturday, Sept. 16, 2017.
Polisi wafanya msako mkali katika eneo la Sunbury-on-Thames, England, Saturday, Sept. 16, 2017.

Polisi nchini Uingereza wamewakamata watuhumiwa wawili Jumatano wanaodaiwa kuhusika na shambulio la bomu la wiki iliyopita katika treni mjini London.

Shambulio hilo lilisababisha zaidi ya watu 30 kujeruhiwa. Maafisa wa usalama wanasema polisi waliwakamata watu hao wenye umri wa miaka 48 na 30 katika mji wa Newport.

Hata hivyo tamko la polisi halikusema jinsi watu hao walivyohusika na shambulio hilo.

“Hili tukio linaendelea kuwa uchunguzi wake ni wa haraka,” amesema Kamanda Dean Haydon, Mkuu wa kituo cha Met cha kupambana na ugaidi,

“Wapelelezi wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina ilikubaini ukweli kamili kuhusu shambulizi hili,”

Kwa jumla kuna watu watano waliokwisha kamatwa kutokana na shambulio hilo lililotokea Ijumaa iliyopita.

Watuhumiwa wote wako rumande na hakuna aliyeshitakiwa mpaka hivi sasa. Kundi la Islamic State limedai kuhusika na shambulio hilo lakini Waziri wa Mambo ya Ndani Amber Rudd amesema halina mashiko.

XS
SM
MD
LG