Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 20:04

Polisi wakamata watu 61 Pakistan kwa sababu ya Khan


23.

Polisi nchini  Pakistan walivamia makazi ya waziri mkuu wa zamani wa taifa hilo,  Imran Khan, katika mji wa mashariki wa Lahore, Jumamosi na kuwakamata watu 61.

Ukamataji huo umetokana na vurugu kati ya polisi na wafuasi wa Khan ambapo iliwalazimu polisi kutumia gesi ya kutoa machozi, kwa mujibu wa polisi.

Afisa wa juu wa polisi Suhail Sukhera ambaye ameongoza operesheni katika kitongoji cha kifahari mjini Lahore, amesema polisi walifanya hivyo ili kuondoa kizuizi kilichowekwa na wanachama wa a chama cha Khan, cha Tahreek-e-Insaf, na wafuasi wengine.

Amesema waliziba barabara za makazi ya Khan kwa kutumia matofali, matawi ya miti yaliyoanguka, mahema na malori yaliyoegeshwa.

Khan hakuwepo nyumbani alikuwa amesafir kwenda Islamabad ambako alitakiwa kufika mbele ya jaji kukabiliana na mashitaka ya kuuza zawadi za serekali wakati alipokuwa madarakani na kuficha mali zake.

Jaji alihairisha shauri hilo mpaka Machi 30.

XS
SM
MD
LG