Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 19:03

Polisi Uturuki wawashikilia darzeni ya walioandamana Sikukuu ya Mei Mosi


Maafisa wa polisi wakilisukuma kundi la waandamanaji, waliokuwa wakijaribu kukaidi katazo la kutoandamana na wakiendelea na maandamano kuelekea Uwanja mkuu wa Taksimu kusherehekea sikukuu ya Mei Mosi, mjini Istanbul, Uturuki, Mei 1, 2022. (Reuters).
Maafisa wa polisi wakilisukuma kundi la waandamanaji, waliokuwa wakijaribu kukaidi katazo la kutoandamana na wakiendelea na maandamano kuelekea Uwanja mkuu wa Taksimu kusherehekea sikukuu ya Mei Mosi, mjini Istanbul, Uturuki, Mei 1, 2022. (Reuters).

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Uturuki wamewakamata darzeni ya waandamanaji waliokuwa wakijaribu kufika katika Uwanja mkuu wa Taksimu mjini Istanbul katika maandamano ya Mei Mosi dhidi ya hali ngumu ya uchumi iliyosababishwa na mfumuko wa bei.

Ofisi ya gavana wa Istanbul ilikuwa imeruhusu maadhimisho ya Mei Mosi yafanyike katika wilaya nyingine na kufanya mikusanyiko katika maeneo yote mengine kuwa ni kinyume cha sheria na haikuruhusiwa.

Mwandishi wa Reuters aliona polisi wakipambana na wakiwafunga pingu waandamanaji, picha ambazo zilionyeshwa katika televisheni na vituo vya ndani vya utangazaji.

Polisi pia waliwakamata watu 30 katika mji wa kati wa Besiktas na wengine 22 katika wilaya za Sisli, Shirika la habari la Demiroren limeripoti.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya gavana wa Istanbul Jumapili imesema kuwa waandamanaji 164 wamekamatwa kote mjini humo kwa “ kujaribu kufanya maandamano kinyume cha sheria.”

Maandamano yalioongozwa na wafanyakazi na jumuiya za wafanyakazi hufanyika wakata wa Mei Mosi kila mwaka kama sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu ya Kimataifa ya Wafanyakazi katika nchi nyingi.

Kiwango cha mfumuko wa bei kwa mwaka nchini Uturuki kinatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 68, kikisukumwa juu na vita vya Russia na Ukraine na kupanda kwa bei za bidhaa, na kitapungua kidogo ifikapo mwisho wa mwaka, utafiti wa Reuters ulionyesha Alhamisi.

Kuongezeka kwa mfumuko wa bei na hali ngumu ya maisha sababu zake zimeelezwa katika taarifa za Mei Mosi zilizotolewa na vikundi mbalimbali.

“Kauli mbiu yetu kuu mwaka huu ilijikita katika gharama za maisha,” mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi vya Uturuki (Turk-Is), Ergun Atalay, alisema wakati akiweka shada la maua katika Uwanja wa Taksim na kushinikiza kuwa kima cha chini cha mshahara cha kila mwezi kirekebishwe kulingana na kupanda kwa bei.

“Mfumuko wa bei unatangazwa kila mwanzo wa mwezi. Kiwango cha mfumuko wa bei lazima kiongezwe katika mishahara kila mwezi,” alisema.

XS
SM
MD
LG