Polisi wa Uturuki wamekamata shehena ya tatu kwa ukubwa ya cocaine katika historia ya nchi hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Yerlikaya alitangaza leo Alhamisi, wakati makundi yanayofuatilia uhalifu wa kupanga yakionya kuwa nchi hiyo imekuwa kituo cha kuingia dawa za kulevya kuelekea Ulaya.
Takribani kilo 608 za cocaine nyingi zikiwa katika mfumo wa maji zilikamatwa katika operesheni kwenye majimbo matatu, Yerlikaya aliandika kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii wa X. Karibu kilo 830 za kemikali zilizotumiwa kusindika dawa hiyo pia zilikamatwa.
Yerlikaya alisema operesheni hiyo ya polisi ililenga genge la kimataifa linalodaiwa kuongozwa na raia wa Lebanon na Venezuela, ambaye alikuwa miongoni mwa wanachama wanne wa kigeni wa kundi la uhalifu wa kupanga, pamoja na Waturuki tisa.
Forum