Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 15:54

Polisi wa Uganda wawakamata waandamanaji wanaopinga kupanda kwa bei ya mafuta na chakula


Rais Yoweri Museveni akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters, Januari 16, 2022.
Rais Yoweri Museveni akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters, Januari 16, 2022.

Polisi wa Uganda walifyatua gesi ya kutoa machozi na kukamata darzeni ya waandamanaji Jumatatu baada ya maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya chakula na mafuta ambayo yaligeuka vurugu.

Taifa hilo la Afrika mashariki lenye watu milioni 45 linakabiliwa na mdororo wa uchumi uliochochewa na janga la Covid 19, na hali hiyo ikazidi kuwa mbaya zaidi kutokana na vita vya Russia nchini Ukraine.

Mfumuko wa bei ya chakula uliongezeka maradufu hadi asilimia 13.1 mwezi Mei, kulingana na takwimu za hivi karibuni za serikali.

Jumatatu, waandamanaji walichoma matairi na kufunga barabara kuu yenye shughuli nyingi huko Jinja, umbali wa kilomita 80 mashariki mwa mji mkuu Kampala, wakiomba serikali kutoa ruzuku ya chakula kinachotumiwa sana.

“Polisi walitumia nguvu za wastani ikiwemo gesi ya kutoa machozi kutawanya waandamanaji, “ msemaji wa polisi katika eneo hilo James Mubi ameiambia AFP.

“Wanane kati ya viongozi wa maandamano hayo wamekamatwa,” amesema, akiongeza kuwa watashtakiwa leo Jumanne kwa kuchochea vurugu.

Waandamanaji walilazimisha waendesha magari kujiunga nao ili kuomba mabadiliko, mashahidi wameiambia AFP.

Bei ya mafuta, chakula na bidhaa msingi zimeongezeka sana ulimwenguni kwa sababu ya vita vya Ukraine, na kuathiri nchi maskini barani Afrika na kwingineko.

Nchini Uganda, lita moja ya petroli inauzwa shilingi 7,000, sawa na dola 1.85, ikiwa imeongezeka mara mbili tangu mwezi Februari. Katika baadhi ya maeneo ya mbali nchini humo, vituo vya mafuta vinauza lita moja hadi shilingi 10,000.

XS
SM
MD
LG