Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 13:25

Polisi wa Sri Lanka wazuia maandamano


Rais mpya wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe, kitia saini hati ya kiapo baada kuapishwa kuwa rais wa Sri Lanka, Alhamisi.
Rais mpya wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe, kitia saini hati ya kiapo baada kuapishwa kuwa rais wa Sri Lanka, Alhamisi.

Vikosi vya Sri Lanka vimetanda katika sehemu kuu za maandamano mjini Colombo, makao makuu ya waandamanaji ambao waliongoza maandamano ya mwezi mzima ya kuipinga serekali.

Hatua hiyo inonekana kama ishara ya rais mpya aliyechaguliwa Ranil Wickremesinghe jinsi atakavyo shughulikia waliofanya kampeni ya kumuondoa mtangulizi wake.

Mamaia vikosi na makamanda wa polisi wakiwa na bunduki na vifaa vya kuliza ghasia walikusanyika nje ya ofisi ya rais katika saa za mapema Ijumaa ili kuwaondoa waandamanaji, ambao walikuwa wakiondoa mahema na mabango nje ya lango kuu la kuingia katika ofisi ya rais.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na polisi imefanyika siku moja baada ya Wickremesinghe kuchaguliwa ambaye pia waandamanaji walipinga asiapishwe.

XS
SM
MD
LG