Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 18:36

Polisi wa serikali ya Ethiopia wapelekwa kwa mara ya kwanza katika jimbo lenye mzozo la Tigray


Wakuu wa majeshi ya Ethiopia na Tigray wabadilishana nyaraka baada ya utiaji saini wa makubaliano ya kusitisha mapigano, Nairobi, Novemba 12, 2022. Picha ya Reuters
Wakuu wa majeshi ya Ethiopia na Tigray wabadilishana nyaraka baada ya utiaji saini wa makubaliano ya kusitisha mapigano, Nairobi, Novemba 12, 2022. Picha ya Reuters

Polisi wa serikali kuu ya Ethiopia wameanza kupelekwa katika mji mkuu wa Tigray Alhamisi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi 18, polisi wamesema, ikiwa hatua ya hivi karibuni kufuatia makubaliano ya amani yaliyosainiwa miezi miwili iliyopita.

Polisi wa serikali kuu, “kulingana na mamlaka waliyopewa na katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia kulinda taasisi za serikali kuu” waliingia Mekele na kuanza kazi,” idara yao imesema katika taarifa kwenye Facebook.

“Watatoa usalama wa kutosha kwa taasisi zinazosimamiwa na serikali kuu, ikiwemo viwanja vya ndege, nishati ya umeme, huduma za mawasiliano ya simu, benki na taasisi nyingine zinazotoa huduma za umma.”

Vita kati ya serikali kuu ya Ethiopia na Tigray vilianza mwezi Novemba mwaka 2020. Waziri mkuu Abiy Ahmed alipeleka wanajeshi ndani ya jimbo hilo la kaskazini baada ya kukishtumu chama tawala katika jimbo hilo, Tigray People’s Liberation Front (TPLF) kushambulia kambi za jeshi la Ethiopia.

Makadirio kuhusu vifo yanatofautiana sana, huku Marekani ikisema watu nusu milioni waliuawa katika vita hivyo.

XS
SM
MD
LG