Mwanamke huyo alishambuliwa mchana kweupe na kundi ka waendesha boda boda baada ya ajali ya barabarani mapema mwezi huu, polisi walisema.
Waendesha boda boda 16 walikamatwa wiki iliyopita baada ya video iliyotanda kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha wanaume hao, wakirarua nguo za mwanamke huyo, huku akipiga kelele za kuomba msaada akiwa ndani ya gari lake na kulazimishwa kufungua mlango wa gari hilo.
Lakini anayedaiwa kuwa kiongozi wa shambulio hilo alitoroka kupitia mfereji wa maji taka na kukwepa kukamatwa hadi Jumatatu, alipotiwa mbaroni katika mji ulio karibu na mpaka wa Tanzania, takriban kilomita 430 kaskazini magharibi mwa Nairobi.
Polisi wamesema “ walimvamia alipojaribu kuvuka mpaka” na kusema kwamba atasafirishwa kwa ndege hadi Nairobi, “ambako atakabiliwa na mkono wa sheria”.