Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:08

Polisi wa Israel wanamchunguza Sara Netanyahu kwa kadhia ya fedha


Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akiwa na mkewe Sara Netanyahu mjini Jerusalem.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akiwa na mkewe Sara Netanyahu mjini Jerusalem.

Ripoti za vyombo vya habari vya Israel zinasema polisi wamependekeza kufunguliwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya mke wa waziri mkuu wa isral, Benjamin Netanyahu kwa shutuma za matumizi mabaya ya fedha za umma kwa makazi rasmi na binafsi.

Sara Netanyahu ambaye anakanusha kufanya makosa yoyote alihojiwa na polisi mwaka jana kuhusiana na uchunguzi wa fedha za umma alizolipwa mhudumu aliyekuwa anamuangalia baba yake kabla ya kifo cha baba huyo.

Uchunguzi ulichochea ukaguzi wa mahesabu ya serikali pia ulilenga kwenye fedha zilizotumika kwa matengenezo ya umeme kwenye nyumba binafsi ya Netanyahu katika eneo la mapumziko la pwani huko Caesarea.

Hakukuwa na ishara yeyote siku ya Jumapili kama waendesha mashtaka watakubali mapendekezo ya polisi.

Msemaji wa waziri mkuu siku ya Jumapili alikanusha kabisa kufanyika kwa kosa lolote. “Haya ni masuala ambayo hata hayakaribii uvunjifu wa sharia”, alisema Nir Hefez katika taarifa yake. “Tuna uhakika kwamba wakati mamlaka itakapoangalia ukweli halili watagundua kwamba hakuna jambo lolote”, alisema.

Sara Netanyahu (L) na mumewe Benjamin Netanyahu huko Jerusalem.
Sara Netanyahu (L) na mumewe Benjamin Netanyahu huko Jerusalem.

Ripoti zinasema uchunguzi huo pia ulichochewa na ushahidi kutoka mlinzi wa zamani katika makazi rasmi ya Netanyahu.

Mapema mwaka huu mlinzi huyo alishinda kesi ya kuumizwa kihisia baada ya mahakama ya kazi kutoa uamuzi kwamba Sara Netanyahu mara kwa mara alimtendea vibaya mkuu huyo na wafanyakazi wengine wa nyumbani.

Moja ya ugunduzi wa mahakama ambao uliungwa mkono na ushahidi ni kwamba Sara Netanyahu wakati mmoja alitupa chini chombo cha kuwekea maua ambapo maua hayo yalikuwa na siku moja tu wakati akimkaripia mfanyakazi huyo na kumueleza kuwa maua hayo si mazuri ya kutosha.

XS
SM
MD
LG