Polisi wa Denmark na Sweden wanasema wamezuia shambulizi la kigaidi jumatano muda mfupi kabla ya kutokea huko Copenhagen na kukamata watu watano ambao walikuwa wamepanga kufanya mauaji ya halaiki.
Shirika la ujasusi la Denmark linasema wanachama wa kundi la wanamgambo wa kiislam wenye msimamo mkali walijaribu kulazimisha kuingia kwenye ofisi za gazeti moja la kila siku la Jyllands Posten na kuuwa watu wengi iwezekanavyo.
Gazeti hilo liliwakasirisha waislam mwaka 2005 kwa kuchora katuni za mtume Muhamad.
Washukiwa wanne kati yao walikamatwa huko Copenhagen. Mtu wa tano alikamatwa Sweden.