Mtu huyo mwenye umri wa miaka 29 alikiri katika uchunguzi uliopewa jukumu la kuwatafuta wahusika wa ajali hiyo ya moto kwamba alihusika kuuanzisha, polisi wamesema katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la Reuters leo Jumatano.
Anatarajiwa kufika mbele ya mahakama ya Johannesburg hivi karibuni kujibu mashtaka ya kuchoma moto, makosa 77 ya mauaji na makosa 120 ya kujaribu kuua, taarifa ya polisi imesema.
Ikiwa moja ya majanga mabaya katika kumbukumbu ya mji huo wa Afrika Kusini ambao ni kitovu cha uchumi, moto huo ulizuka tarehe 31 Agosti 2023 katika jengo bovu lililojaa wahamiaji wengi wa kigeni.
Wengi kati ya waathirika waliungua vibaya kiasi cha kutotambulika.
Forum