Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 14:34

Polisi Ujerumani walivunja maandamano yanayounga mkono Palestina


Polisi wa Ujerumani wakishuhudia maandamano yanayounga mkono Palestina.
Polisi wa Ujerumani wakishuhudia maandamano yanayounga mkono Palestina.

Waandamanaji waliweka kiasi cha mahema 20 na walishikana mikono kuunda mstari mrefu kuzunguka mahema

Polisi wa Ujerumani leo Jumanne walivunja maandamano ya mamia ya wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina ambao walikuwa wamekaa kwenye uwanja katika chuo kikuu cha Free mjini Berlin mapema leo hatua ya hivi karibuni kama hiyo ya mamlaka wakati maandamano ambayo yametikisa vyuo vikuu nchini Marekani yakienea kote Ulaya.

Waandamanaji waliweka kiasi cha mahema 20 na walishikana mikono kuunda mstari mrefu kuzunguka mahema. Wengi walikuwa wamefunika nyuso zao kwa barakoa za matibabu na walikuwa wamevaa kofia vichwani mwao, wakipiga kelele kama vile "Viva, viva Palestina."

Mapema Jumanne, polisi wa Uholanzi waliwakamata wanaharakati wapatao 125 wakati walipovunja kambi kama hiyo, ya maandamano ya Wapalestina katika Chuo Kikuu cha Amsterdam.

Forum

XS
SM
MD
LG